Masharti ya Matumizi
Imesasishwa 31 Oktoba 2026
1. Kukubali masharti
Kwa kujisajili, kununua kifurushi, kutumia vocha au kuunganishwa na mtandao wa YetuNet, unakubali Masharti haya na Sera ya Faragha. Kama hukubali, usitumie huduma.
2. Huduma
Tunauza vifurushi vya Wi-Fi vya muda au data, na intaneti ya kila mwezi. Kila kifurushi kina muda, kiasi cha data, kasi na idadi ya vifaa vinavyoruhusiwa kama vilivyoonyeshwa kwenye app kabla ya kununua.
3. Akaunti yako
- Toa taarifa sahihi na uzisasishe.
- Linda nenosiri lako na namba za kuthibitisha (SMS code). Usimpe mtu yeyote — wafanyakazi wetu hawatakuomba nenosiri.
- Unawajibika kwa kila kinachofanywa kupitia akaunti, vocha au kifaa chako.
4. Malipo na kurudishiwa pesa
- Bei ni kama zinavyoonyeshwa kwenye app au tovuti wakati wa kununua.
- Kifurushi kilichokwisha anza kutumika hakirudishwi wala pesa kurudishwa, isipokuwa pale huduma ilishindwa kwa sababu ya upande wetu.
- Malipo yaliyokatwa bila kifurushi kutolewa yatashughulikiwa ukiwasiliana nasi na kumbukumbu ya muamala.
- Kwa kukatika kwa muda mrefu tunaweza kutoa fidia ya muda kwa uamuzi wetu.
5. Matumizi yasiyoruhusiwa
Hairuhusiwi kutumia mtandao wetu:
- kufanya jambo lolote kinyume cha sheria za Tanzania, ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, 2010;
- kusambaza au kutazama picha za unyanyasaji wa watoto, maudhui ya chuki, vitisho au uchochezi;
- udukuzi, kuvamia mifumo, kusambaza virusi, spam au utapeli;
- kupakua au kusambaza kazi zenye hakimiliki bila ruhusa;
- kuuza tena huduma, au kuitumia kwenye vifaa zaidi ya vinavyoruhusiwa na kifurushi;
- kuvuruga mtandao au watumiaji wengine;
- kubadilisha anwani ya kifaa, kutumia namba au simu nyingi, au mbinu nyingine kukwepa malipo au kupata offer zaidi ya mara moja.
6. Matumizi ya haki (fair use)
Kwa vifurushi vyenye "matumizi ya haki", kasi inaweza kupunguzwa baada ya kiasi kilichoonyeshwa, ili kila mteja apate huduma nzuri.
7. Wajibu wako kwa matumizi yako
Unawajibika kikamilifu kwa kila unachofanya mtandaoni kupitia muunganisho wako. YetuNet ni njia ya kukufikisha kwenye intaneti tu: hatutawajibika kwa matumizi mabaya ya intaneti, kwa maudhui unayotazama, kupakua au kutuma, kwa makosa au uhalifu unaofanywa kupitia muunganisho wako, wala kwa madhara yoyote yanayotokana nayo. Utatufidia kwa madai, hasara au gharama zozote zitakazotokana na matumizi yako mabaya au kuvunja Masharti haya.
8. Upatikanaji wa huduma na usumbufu
Tunajitahidi huduma ipatikane wakati wote, lakini inatolewa "kama ilivyo". Kukatika au kupungua kwa kasi kunaweza kutokea kwa sababu ya umeme, hali ya hewa, mtoa huduma wetu wa juu, matengenezo, wizi au uharibifu wa vifaa, maagizo ya mamlaka, au sababu nyingine zilizo nje ya uwezo wetu.
Hatutawajibika kwa usumbufu wowote unaoweza kutokea (ikiwemo kukatika, kuchelewa au kupungua kwa kasi), kupoteza data, kazi, biashara au faida, wala madhara yasiyo ya moja kwa moja. Kwa vyovyote vile, kiwango cha juu cha uwajibikaji wetu ni kiasi ulicholipa kwa kifurushi husika.
9. Tovuti na huduma za watu wengine
Hatudhibiti wala kuwajibika kwa tovuti, app au huduma za watu wengine unazofikia kupitia mtandao wetu.
10. Usalama wa kifaa chako
Mtandao wa Wi-Fi ni wa umma. Linda kifaa chako kwa nenosiri, sasisha mfumo wake, na usitume taarifa nyeti kwenye tovuti zisizo salama (zisizo na "https").
11. Offer na zawadi
Offer ni zawadi tunayotoa kwa hiari yetu: hutolewa mara moja kwa kila kipindi kwa kila namba ya simu na kwa kila simu, na tunaweza kuibadilisha au kuisimamisha wakati wowote. Kujaribu kudanganya mfumo kupata offer zaidi kutasababisha offer kufutwa na akaunti kusimamishwa.
12. Kusimamisha huduma
Tunaweza kusimamisha au kufunga akaunti, vocha au kifaa kinachovunja Masharti haya, bila fidia, na kutoa taarifa kwa mamlaka pale inapohitajika.
13. Sheria inayotumika
Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na migogoro itaamuliwa na mahakama za Tanzania.
14. Mabadiliko
Tunaweza kubadilisha Masharti haya. Tukibadilisha kitu cha msingi tutakujulisha ndani ya app na kukuomba ukubali tena.
Wasiliana nasi
- Simu: +255 687 706 155
- WhatsApp: +255 687 706 155
- Barua pepe: [email protected]
- Sinoni Area, Arusha