Sera ya Faragha
Imesasishwa 31 Oktoba 2026
1. Sisi ni nani
YetuNet ni mtoa huduma ya intaneti (Wi-Fi ya vifurushi na intaneti ya kila mwezi) — Arusha, Tanzania. Sera hii inaeleza taarifa tunazokusanya unapotumia mtandao wetu, tovuti yetu na app ya mteja, kwa nini tunazitumia, na haki zako chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022.
2. Taarifa tunazokusanya
- Unazotupa wewe: jina, namba ya simu, barua pepe, jina la mtumiaji na nenosiri (nenosiri huhifadhiwa likiwa limefichwa — hatuwezi kulisoma), maombi ya msaada na ujumbe unaotutumia.
- Malipo: namba ya mobile money uliyolipia, kiasi, kumbukumbu ya muamala na hali yake. Hatuoni wala kuhifadhi PIN yako. Malipo hufanywa na M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa kupitia mtoa huduma wa malipo.
- Matumizi ya mtandao: anwani ya kifaa (MAC address), anwani ya IP tunayokipa kifaa, muda wa kuunganishwa na kukatika, kiasi cha data ulichotumia, na kituo (router) ulichounganishwa nacho. Hatusomi maudhui ya unachotuma au kupokea, na hatuhifadhi orodha ya tovuti unazotembelea.
- Simu na app: aina ya simu na mfumo wake kama browser inavyoviripoti (mfano "Android 14 · SM-A155F"), namba ya siri ambayo app hujitengenezea na kuihifadhi kwenye simu yako (kwetu huhifadhiwa ikiwa imefichwa), kama app imesakinishwa, na lugha au mwonekano uliouchagua.
- Usalama: muda na IP ya kuingia kwenye akaunti, na majaribio ya kuingia yaliyoshindwa.
3. Ruhusa za simu (permissions)
App ya YetuNet ni app ya wavuti (web app). Haiwezi kusoma IMEI, namba ya serial, MAC address halisi ya simu, ujumbe wako wala orodha ya simu ulizopiga. Ruhusa inazoweza kuomba ni hizi tu, na zote ni za hiari:
- Arifa (Notifications): kukujulisha kifurushi kinapokaribia kuisha, malipo yanapopokelewa na offer mpya. Unaweza kuzizima wakati wowote kwenye mipangilio ya simu.
- Kamera: pale tu wewe mwenyewe unapobonyeza kupiga picha — mfano picha ya tatizo kwenye ombi la msaada au kuskani QR ya vocha. Hatuwashi kamera bila wewe.
- Picha na faili: pale tu unapochagua picha mwenyewe — mfano picha ya wasifu au ushahidi wa tatizo/malipo. Hatusomi gallery yako.
- Anwani (Contacts): hatusomi wala kupakia orodha yako ya anwani. Tukiongeza "Mwalike rafiki" siku zijazo, utachagua mwenyewe anwani moja kwenye dirisha la simu, na tutatumia namba hiyo tu kumtumia mwaliko — kamwe si orodha nzima. Tutasasisha sera hii na kukuomba ukubali kabla ya hapo.
- Mahali (GPS): hatukusanyi mahali ulipo kwa GPS. Tunajua eneo kwa kadiri ya kituo cha Wi-Fi ulichounganishwa nacho.
- Intaneti: app inahitaji intaneti. "Speed test" hutuma na kupokea data kwenda server zetu tu.
4. Kwa nini tunatumia taarifa hizi
- Kukupa huduma: kukuunganisha, kuhesabu muda na data, kukuonyesha salio, vifaa na matumizi yako.
- Malipo, risiti na ankara.
- Kukusaidia unapotuomba msaada.
- Offer na zawadi: tunatumia namba yako ya simu pamoja na namba ya siri ya app ili offer itolewe mara moja kwa kila kipindi kwa kila namba na kwa kila simu, isijirudie na isitumiwe vibaya.
- Usalama na kuzuia udanganyifu (mfano kujaribu kupata offer mara nyingi kwa namba au simu tofauti).
- Kuboresha mtandao kwa takwimu za jumla.
- Ujumbe wa huduma kwa SMS (namba za kuthibitisha, risiti, ukumbusho). Ujumbe wa matangazo hutumwa tu kama hujakataa, na unaweza kuacha wakati wowote.
- Kutimiza matakwa ya sheria.
5. Tunawashirikisha nani
Hatuuzi taarifa zako. Tunazishirikisha tu kwa kiasi kinachohitajika na: watoa huduma za malipo, mtoa huduma wa SMS, mtoa server tunayotumia, na mamlaka za kisheria (mfano TCRA, Polisi au Mahakama) pale sheria inapotutaka kufanya hivyo.
6. Muda wa kuhifadhi
- Taarifa za akaunti: muda wote akaunti iko hai, na hadi miezi 12 baada ya kuifunga.
- Kumbukumbu za malipo: kwa muda unaotakiwa na sheria za kodi na biashara.
- Kumbukumbu za kuunganishwa (MAC, IP, muda, data): kwa muda unaotakiwa na sheria, kisha hufutwa.
- Kumbukumbu za simu iliyotumia app: hufutwa baada ya miezi 12 bila kutumika.
7. Usalama wa taarifa
Tunatumia muunganisho uliosimbwa (HTTPS), nenosiri lililofichwa, ruhusa kwa wafanyakazi wanaohitaji tu, na kumbukumbu ya kila hatua muhimu (audit log). Hakuna mfumo usio na hatari kabisa; tukigundua uvujaji unaokuhusu tutakujulisha na kuiarifu mamlaka kama sheria inavyotaka.
8. Haki zako
Chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 una haki ya: kujua taarifa tulizonazo kukuhusu, kupata nakala yake, kuzisahihisha, kuomba zifutwe pale sheria inaporuhusu, kukataa ujumbe wa matangazo, na kuondoa ridhaa yako. Wasiliana nasi kwa maelezo yaliyo hapa chini. Usiporidhika, unaweza kulalamika kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
9. Watoto
Akaunti ni kwa watu wenye miaka 18 au zaidi. Aliye chini ya miaka 18 atumie huduma kwa ridhaa na usimamizi wa mzazi au mlezi.
10. Mabadiliko ya sera hii
Tukibadilisha kitu cha msingi tutakujulisha ndani ya app na kukuomba ukubali tena kabla ya kuendelea.
Wasiliana nasi
- Simu: +255 687 706 155
- WhatsApp: +255 687 706 155
- Barua pepe: [email protected]
- Sinoni Area, Arusha